This site uses technical (necessary) and analytics cookies.
By continuing to browse, you agree to the use of cookies.

Celebrating World Kiswahili Language Day

WhatsApp Image 2024-07-12 at 13.10.02

Today, on World Kiswahili Language Day, the Embassy of Italy is pleased to confirm its commitment to promoting the Swahili language in the framework of the excellent Italian-Tanzanian relations.

We are happy to inform that we are introducing Kiswahili into all our online platforms to enrich our bilateral relations also through the beauty and popularity of this unique language.

We also seize this opportunity to recall some recent initiatives, two of which are by Mrs. Michelangela Adamo, who worked at the Italian Embassy for several years.

Tumia Akili” is an engaging educational game designed to enrich Kiswahili learning among youth. “Hadithi kwa njia ya simu” is the translation into Swahili of 30 fairy tales by Gianni Rodari.

Almawave, a leading Italian company in the field of artificial intelligence, has developed extensive expertise over the years in translating and transcribing judicial procedures in Tanzania also in Kiswahili. The company recently launched Velvet, an open-source Large Language Model (LLM), aimed at enhancing the understanding and generation of natural language also for Swahili speakers, in order to reduce linguistic barriers and provide to the general public high-quality support in Kiswahili.

 


Leo, ni Siku ya Lugha ya Kiswahili Duniani. Ubalozi wa Italia unafuraha kubwa kutangaza dhamira yake ya kukuza lugha na utamaduni wa Kiswahili kudimisha mahusiano bora ya nchi za Italia na Tanzania.

Tunayo furaha kuwajulisha kwamba kuanzia sasa, tunaongeza machapisho kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika majukwaa yetu yote ya jamii ili kuimarisha zaidi uhusiano wetu baina ya nchi hizi mbili, na kutangaza uzuri na umaarufu wa lugha hii ya kipekee.

Pia, katika hili, tunachukua fursa hii kuwakumbusha hapo awali, juhudi za Bi.  Michelangela Adamo, Mfanyakazi Mstaafu alie fanya kazi Ubalozi wa Italia kwa miaka mingi. “Tumia Akili” mchezo unaovutia wa elimu, ulioundwa ili kuboresha ufundishaji wa lugha ya Kiswahili kwa vijana. Pamoja na, “Hadithi kwa njia ya simu” tafsiri ya hadithi 30 za Gianni Rodari kwa lugha ya Kiswahili.

Almawave, kampuni ya Ki Italiano inayo ongoza katika nyanja ya akili bandia, imeonyesha utaalam mkubwa kwa miaka mingi katika kutafsiri na kuhakiki taratibu za mahakama nchini Tanzania kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza. Ustadi wa kampuni hii katika teknolojia ya sauti umekuwa muhimu katika kuongeza ufanisi na uenezaji wa mifumo ya mahakama za Tanzania, na kuhakikisha huduma sahihi na za haraka za unukuzi na tafsiri. Hivi karibuni, kampuni imezindua Velvet, mfano wa lugha kubwa wa chanzo wazi (LLM). Mradi huu bunifu unawakilisha hatua muhimu mbele katika teknolojia ya modeli ya lugha. Mpango huo unalenga kuongeza uelewa na uzalishaji wa lugha asilia kwa wazungumzaji wa Kiswahili ili kupunguza vizuizi vya lugha na kutoa usaidizi wa hali ya juu wa lugha ya Kiswahili, kukuza ushirikishwaji na uwezeshaji wa kidijitali.